TRENI ambayo ilikuwa na kichwa kimoja ikielekea kuchukua mabehewa imegongwa na gari kubwa ya mizgo eneo la karume jijini dar na kusababisha foleni ndefu katika eneo hilo
Tukio hili limejiri leo asubuhi ya saa 12 alfajiri ambapo gari
hilo lilikuwa likipita kwa kasi kubwa bila kufuata alama za barabarani zinazoonyesha sehemu ya reli
Ofisa oparesheni wa shirika la reli, Mohamed Kanka , alisematreni hiyo ilikuwa ikipita majira ya saa kumi na mbili alfajiri na kugongwa na gari iliyokuwa ikipita pasipo dereva wa gari hiyo kuzingatia alama iliyokuwa ikionyesha kuwa sehemu hiyo kuna reli.
Alisema kuwa katika ajali hiyo dereva wa gari na dereva aliyekuwa katika treni wameumia na wamekimbizwa katika hospitali ya aman Ilala kwa ajili ya kupatiwa matibabu.
vilevile alisema baada ya ajali hiyo kutokea, gari jengine lililokuwa limesimama liligongwa na kichwa cha treni baada ya kuiacha njia yake na kuelekea uande wa magari yaliyokuwa yakipaki.
Ofisa huyo amewaasamadereva kuwa makini wanapofika eneo lenye alama kuonyesha mbele kuna reli kwani ajali nyingi hutokea kutokana na madereva wasiokuwa waangalifu.
No comments:
Post a Comment