FAHAMU SAIKOLOJIA YA JINSIA NA MAHUSIANO YA KIMAPENZI KWA UNDANI, ITAKUSAIDIA KUJITAMBUA NA KUMTAMBUA MWENZI WAKO. MWANAUME IN NANI KATIKA JAMII?

1. Ni kiongozi wa familia
2. NI mlinzi wa mwanamke pamoja na familia
3. NI mfano wa kuigwa na jamii
4. Ni mrithi wa Mungu
MWANAUME MWENYE MAADILI
- NI mnyenyekevu wakati wote
- Ni mvumilivu wakati wote
- Yupo tayari kusuluhisha kesi yake na kuanza upya
- Ni mwepesi kusamehe na kusahau
- Ni mtu mwenye utu na anathamini utu wa mtu
- Anajali watoto na mke wake
- Hata kama sio mwaminifu hujitahidi sana mke wake asijue
MWANAUME ASIYE NA
MAADILI
- Mkorofi kupindukia

- Hana utu wala kujali
- Ni mtu wa lawama wakati wote
- Hana hofu kwa chochote anachokifanya
- Huhesabu makosa wakati wote
- Hana maneno ya faraja kila wakati kulaani tu
- Hana moyo wa kusamehe, sio rahisi kesi yake imalizike kwa amani
MWANAMKE NI NANI KATIKA JAMII?
1. Ni msaidizi mwa mwanaume
2. Ni taji ya mwanaume
3. Ni mjenzi wa mji wake na nyumba yake
4. Ni kipenzi cha watoto na mume wake
5. Ni mwalimu wa familia
6. NI mshawishi wa tabia njema kwa jamii inayomzunguka
MWANAMKE MWENYE MAADILI
- Hana haraka ya mambo
- Mvumilivu, mnyenyekevu, mtiifu, mkweli, anaheshima, anajituma, ana utu
- Yuko tayari kufanya suluhu na kusahau
- Yuko tayari kujifunza kutokana na makosa
- Ana mapenzi ya dhati na ya kweli
- Anajali watoto na mume wake pamoja na jamii inayomzunguka
- Hayuko tayari kumsaliti mume wake hata kama sababu zote anazo
MWANAMKE ASIYE NA MAADILI
- Ni mkorofi
- Ana hasira kwa karibu sana na za wazi wazi sana
- KInywa chake huwa na matusi na lawama kila wakati
- Hukusanya makosa ya mume wake wakati wote
- Huwa na upendi wa mitego, hana upendo wa dhati
- Hulazimisha mambo yafanyike hata kama haiwezekani kwa wakati huo.
Hapo mwanaume unapopata mke mwenye tabia njema au mke kupata mume mwenye tabia njema ndoa yenu inakuwa yenye amani kubwa na kufanyika kimbilio kwa wengine, lakini pindi inapotokea mume/mke mwenye maadili mema akapata mwenzi asiyekuwa na maadili mema inakuwa ni vigumu na taabu nyingi kwenye ndoa, na itachukua muda mrefu sana kumbadilisha mwenzi wako awe katika mstari sahihi.
Ndio maana inashauriw kwamba kabla ya kufunga ndoa unapaswa kuyatazama haya kwa undani sana itakusaidia. CHUKUA TAHADHARI MAPEMA KABLA YA HATARI.

No comments:

Post a Comment