Treni ya kisasa (Delux), kwenda Bara yenye mabehewa 22 imeanza safari kwenda Kigoma

Treni ya kisasa (Delux), kwenda Bara yenye mabehewa 22 ilianza safari yake yasaa 30 kutoka Dar es Salaam kwenda Kigoma ikiwa ni tofauti ya saa sita ikilinganishwa na safari ya treni ya zamani.Kutokana na tofauti hiyo, abiria walioanzasafari kwa furaha na matumaini jana saa tano asubuhi wanatarajiwa kufika Kigomaleo saa 11 jioni badala ya saa tano usiku.Hata hivyo, abiria hao watalazimika kuingiza mikono yao zaidi
mifukoni, kutokana na kiwango kipya cha nauli kuwa Sh79,400 badala ya Sh75,700 za awali kwa daraja la kwanza.Huku nauli za daraja la pili ikishuka kutoka Sh55,400 hadi Sh,47,600 zile za daraja la tatu zimepanda kutoka Sh27,700hadi Sh35,700.

No comments:

Post a Comment