HUKU AKISAKWA KUMPASUA MTU KICHWA TID AMPIGA MENEJA WAKE


Pepo la ugomvi lazidi kumuandama staa wa bongo fleva Khalid Mohamed TID baada ya kusakwa na jeshi la polisi kwa kosa la kumjerui mtu wiki iliyopita msanii huyo  ametengeneza
kichwa cha habari kwa mara nyingine akidaiwa kumpiga meneja wake aliyefahamika kwa jina la tall myama
STAA WA BONGO FLEVA  TID

Katika tukio la awali TID alidaiwa
alitembeza kichapo na kumjeruhi bw.james richard  kwa kosa la kupaki gari katika eneo lake maeneo ya nyumbani kwake kinondoni-sterio jijini dar

Tukio la kumpiga meneja wake TID anadaiwa kulifanya katika hotel ya Element oystabey ambapo inaelezwa kuwa msanii huyo alifika hotelini hapo akiwa na wapambe wake, na alimkuta meneja wake alibishana nae kwa muda mfupi  kisha akamzaba kibao.

Alimkuta mwenzake(Tall) kakaa sehemu,akamsemesha na alipojibu tu akamzaba kofi, lakini meneja wake alikuwa mstaarbu  hakumlipizia, baada ya tukio hilo TID alitokomea na kama unavyojua kuwa sasa hivi anaishi kama digidigi, asipompiga mtu hasikii raha. kilidai chanzo chetu

chanzo hicho kilizidi kumwaga "mchele" kuwa baada ya meneja huyo kupokea kipigo alienda kutoa taarifa kituo cha polisi oystabey kilicho chini ya Camillius Wambura (pichani) ambapo lilifunguliwa jarada
RPC Camillius Wambura

na meneja huyo alikiri kutokea kwa tukio hili akasema hakutaka kulivalia njuga jambo hilo ila alichokifanya ni kutoa taarifa polisi endapo atarudia amchukulie hatua kali zaidi



ni kweli TID alinishambulia kwa kunipiga kibao iliniuma sana ila niliamua kumsamehe, nilichokifanya ni kutoa taarifa kituo cha polisi ili kama atarudia nimchukulie hatua kali "Alisema meneja huyo"
































No comments:

Post a Comment