Askofu gwajima kaenda polisi dar mwenyewe alichosema.....kiko hapa>>>>

Miongoni mwa taarifa zilizochukua Headlines
katika taarifa ya Habari ya kituo cha ITV ni hii ya
Kiongozi wa Kanisa la Ufufuo na Uzima,
Askofu Josephat Gwajima ambae
amefika kituo
kikuu cha Polisi Dar kwa ajili mahojiano na Jeshi
la Polisi kwa madai ya kutoa kauli yenye maneno
makali kwa kiongozi wa Kanisa
Katoliki, Askofu Kardinali Pengo.
Askofu Gwajima amesema maneno aliyoyatoa ni
ya kumkemea kiongozi mwenzake wa kiroho kwa
madai ya kukiuka msimamo wa viongozi wenzie
wa dini wa kukataa Mahakama ya Kadhi.
“Baraza la Maaskofu Tanzania waliamua kwa
pamoja na wakasaini waraka kwa pamoja,
kwamba hawataki Mahakama ya Kadhi… lakini
tukashangaa mwenzetu Askofu Pengo aliyesaini
na yeye anageuka sasa tukajiuliza kwa nini
anageuka? mimi kama kiongozi wa kiroho nikaona
nimkemee.. lakini nimeitwa na Polisi sasa najiuliza
niliyemkemea ni Polisi au nilimkemea nani? “ –
Askofu Gwajima.
Hivi karibuni katika mitandao ya kijamii kumezagaa
picha za video zenye maneno ya kashfa kwenda
kwa kiongozi wa Kanisa Katoliki Askofu Kardinali
Pengo jambo lililofanya jeshi la Polisi kumtaka
afike kituoni kikuu cha Polisi kwa mahojiano.

No comments:

Post a Comment